Advertisement
KANDANDA:

Da Rosa atajwa kumalizana na Singida FG

Da Rosa ana uzoefu mkubwa wa kufundisha soka la Kiafrika kwani aliwahi kuzinoa timu kama Rayon Sports, Coton Sports, CS Constantine, Horoya AC, Al-Merreikh pamoja na timu ya Taifa ya Mauritania.
Advertisement

ALIYEKUWA Kocha wa timu ya Simba, Mreno Didier Gomes da Rosa, anatajwa kuwa kocha mpya wa timu ya Singida Fountain Gate baada ya kukubaliana nao kila kitu.

Advertisement

Da Rosa, 53 ambaye alizaliwa Ufaransa, aliwahi kuhudumu ndani ya Simba mwaka 2021 lakini hakumaliza msimu alitimuliwa.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka ndani ya Singida Fountain Gate, zimedai pande hizo mbili zimeshafikia makubaliano na wakati wowote watamtangaza.

Kocha huyo atakwenda kuvaa viatu vilivyoachwa na Mjerumani Ernst Middendorp ambaye alihudumu ndani ya timu hiyo kwa wiki mbili na kuachia ngazi.

Advertisement

Middendorp aliiongoza Singida FG katika mchezo mmoja wa kimashindano wa Kombe la Shirikisho na kushinda bao 1-0, lakini saa chache baadaye alitangaza kujiuzulu na kutimikia Afrika Kusini.

Mjerumani huyo alirithi mikoba kutoka kwa Mholanzi, Han van Pluijm ambaye aliiwezesha timu hiyo kushika nafasi ya nne katika Ligi Kuu Bara msimu uliopita na kufuzu kucheza michuano ya kimataifa.

Taarifa zaidi kutoka ndani ya Singida FG, zinadai kocha huyo amekubali kuachana na timu yake aliyokuwa akiinoa ya Al-Taraji ya Saudi Arabia na kujiunga nayo kutokana na kupenda kufundisha soka la Tanzania.

Advertisement

Da Rosa ana uzoefu mkubwa wa kufundisha soka la Kiafrika kwani aliwahi kuzinoa timu kama Rayon Sports, Coton Sports, CS Constantine, Horoya AC, Al-Merreikh pamoja na timu ya Taifa ya Mauritania.

Alipotafutwa Ofisa Habari wa Singida FG, Hassan Massanza kuzungumzia hilo, amesema suala hilo halijafika mezani kwake ila atalifuatilia kujua kinachoendelea ila kwasasa timu ipo chini ya Kocha, Mrundi Ramadhani Nsanzwirimo.

Advertisement
Advertisement
More from Pulse Sports Uganda