Advertisement
KANDANDA

Dabo ajivunia 'majembe' aliosajili dirisha dogo

Kocha wa Azam FC, Yusuph Dabo (kushoto), akiwa na msaidizi wake, Bruno Ferry
Huyo ni Kocha wa Azam FC ambaye ameiongoza timu hiyo hadi sasa kukaa kileleni katika msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara
Advertisement

Kocha Mkuu wa kikosi cha Azam FC, Yusuph Dabo, amesema wachezaji aliosajili katika dirisha dogo wote ni balaa na hivyo watu wawape muda tu kabla ya kuanza kuwafaidi.

Advertisement

Dabo ameyasema hayo wakati akizungumza na Pulsesportsambapo ameshangazwa na uwezo mkubwa ambao wanaonesha nyota hao wapya kikosini.

Katika dirisha la usajili dogo ambalo lilifungwa mwezi uliopita, Azam ilisajili wachezaji watatu ambao ni Kipa, Mohamed Mustapha raia wa Sudan ambaye alitoka katika timu ya El-Marekh.

Wengine ni kiungo mshambuliaji, Franklin Navarro na beki wa kati, Yeison Fuentes kutoka Leones na wote hao wakiwa ni raia wa Colombia.

"Nimevutiwa na wachezaji wapya ambao wamejiunga na sisi katika usajili wa dirisha dogo, nilichopenda zaidi kwanza ni vijana wadogo lakini wana ubora wa hali ya juu, watahitaji muda zaidi wa kuzoea mazingira lakini nadhani watu watawafaidi," amesema Dado.

Advertisement

Azam ambao ni vinara wa ligi, wapo katika kampeni yao ya kutaka kulinyakuwa taji la ligi kwa mara ya kwanza baada ya kupita miaka 11.

Kikosi chao kwasasa kipo mawindoni kikijiandaa na mechi yao inayofuata Februari 9 ambapo itacheza dhidi ya Simba katika Uwanja wa Azam Complex.

Kwa mujibu wa kocha Dabo, amesema maandalizi yao yanakwenda kama walivyopanga na anafurahi kupata baadhi ya mechi za kirafiki ikiwemo ile dhidi ya KVZ ambayo walishinda 3-1.

Advertisement
Advertisement
More from Pulse Sports Uganda