Advertisement
KANDANDA

Inonga aongeza mzuka Simba SC ikijiandaa kuivaa Asec Mimosa

Timu hizo zinatarajia kuumana Februari 24 katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika
Advertisement

Beki wa kimataifa wa DR Congo,Henock Inonga, ameungana na wachezaji wenzake kambini kujiandaa na mchezo dhidi ya Asec Mimosa ya Ivory Coast wa Ligi ya Mabingwa Afrika.

Advertisement

Mchezo huo wa Kundi B unatarajiwa kuchezwa Februari 24 na timu hiyo ina nafasi ya kusonga hatua ya robo fainali ya michuano hiyo.

Inonga ambaye amekosekana katika mechi Tano za michuano mbalimbali tangu Ligi Kuu Bara ilivyosimama na kisha kurejea kupisha michuano ya AFCON, ameanza mazoezini binafsi kabla ya kuungana na wenzake.

Inonga alikuwa sehemu ya kikosi cha DR Congo ambacho kilishika nafasi ya nne katika michuano ya AFCON baada ya kufungwa na Afrika Kusini katika mchezo wa kuwania mshindi wa tatu.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Klabu yake ya Simba kupitia kurasa zao za mitandaon ya kijamii, imememuonesha beki huyo akifanya mazoezi tofauti tofauti.

Advertisement

Pamoja na kuweka picha za aina tofauti tofauti, imeambatanishwa na maelezo ambayo yamesomeka:" Beki la Afcon limetua na kuanza mazoezi".

Simba leo ilitakiwa kuwa uwanjani kuumana na Mtibwa Sugar katika mchezo uliotakiwa kuchezwa Uwanja wa Jamhuri, Morogoro lakini uliahirishwa ili kutoa nafasi kwa timu hiyo kujiandaa na mechi za kimataifa.

Katika michuano hiyo ya kimataifa, Simba inashika nafasi ya pili ikiwa na alama 5 nyuma ya Asec Mimosa yenye alama 10, Galaxy ina alama 4 na Wydad alama 3.

Advertisement
Advertisement
More from Pulse Sports Uganda