Advertisement
KANDANDA

JKT Tanzania, Simba SC ni kivumbi na jasho leo jeshini

Ni mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara ambao utakuwa unafungwa mechi za mzunguko wa kwanza
Advertisement

Kocha Msaidizi wa timu ya Simba SC, Daniel Cadena, amesema wanataka kushinda mchezo wao wa Ligi Kuu Bara dhidi ya JKT Tanzania leo ili kujisogeza karibu na wapinzani wao Yanga katika mbio za ubingwa msimu huu.

Advertisement

Mchezo huo wa kufunga mzunguko wa kwanza kwa timu zote, unatarajiwa kuchezwa saa 10 jioni Uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo, Dar es Salaam.

Akizungumza jijini Dar es Salaam kuelekea mchezo huo, Cadena amesema kwasasa dhumuni lao kwenye kila mechi ni kuvuna alama tatu ili wasitoe nafasi ya kuachwa alama nyingi na wapinzani wao katika mbio za ubingwa.

Amesema anajua mchezo dhidi ya JKT Tanzania utakuwa ni mgumu hasa kwakuwa timu hiyo ipo kwenye uwanja wao wa nyumbani lakini wao wamejiandaa ili kushinda.

“Tunataka kuwa karibu na wapinzani wetu na ili kufanya hivyo lazima tushinde kwenye mechi zetu, mchezo wa kesho (leo) ni mgumu hasa kwakuwa tutakuwa ugenini lakini hatuna budi zaidi ya kushinda,” amesema.

Advertisement

Aidha kocha Cadena amebainisha kuelekea mchezo huo kuwa kikosi chao kipo kamili, wachezaji wote wanatarajia kuwa sehemu ya mchezo isipokuwa Willy Onana na Aubin Kramo ambao bado wanauguza majeraha.

Simba ipo nafasi ya pili katika msimamo wa ligi hiyo wakiwa na alama 33 ambazo ni saba nyuma ya vinara Yanga.

Katika hatua nyingine, Kocha Cadena, amewatoa hofu mashabiki wa Simba kwa kuwaambia kuwa washambuliaji wao wapya watafunga mabao ya kutosha msimu huu.

Amesema washambuliaji waliowasajili katika dirisha dogo ambao ni Freddy Michael Koublan na Pa Omar Jobe ni wachezaji wa daraja la juu na hivyo ni suala la muda tu kama ya kuanza kuonesha mavitu yao ndani ya ligi.

Koublan na Jobe kila mmoja ana bao moja katika mechi nne za ligi kuu ambazo wamezicheza tangu wakamilishe usajili wa kujiunga na Simba katika usajili uliopita.

Advertisement

Mechi zingine;

Tanzania Prisons v Singida FG

Coastal Union v Dodoma Jiji

Advertisement
Advertisement
More from Pulse Sports Uganda