Rais Dkt. Samia aagiza ujenzi viwanja viwili

© Kwa Hisani

KANDANDA Rais Dkt. Samia aagiza ujenzi viwanja viwili

Zahoro Mlanzi • 12:32 - 28.09.2023

Rais Samia amewapongeza wote walioshiriki kuhakikisha Tanzania inapata fursa ya kushiriki michuano hiyo.

Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, ameiagiza Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo kufanya maandalizi ikiwemo kukamilika kwa wakati na kwa ubora wa hali ya juu viwanja viwili vipya vya kisasa vya michezo Arusha na Dodoma.

Maagizo hayo yamekuja baada ya leo Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) kupitisha ombi la nchi za Kenya, Uganda na Tanzania kuandaa fainali za kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) kwa mwaka 2027.

“Tunamshukuru Mwenyezi Mungu tumefanikiwa kuwa wenyeji wa michuano mikubwa ya soka Afrika (AFCON2027), tukishirikiana na Kenya na Uganda.” ameandika Rais Samia kupitia mtandao wa X.

Rais Samia amewapongeza wote walioshiriki kuhakikisha Tanzania inapata fursa ya kushiriki michuano hiyo.