Advertisement
KANDANDA

Taifa Stars yapiga tizi mara mbili Ivory Coast

Wachezaji wa Taifa Stars wakiwa mazoezini nchini Ivory Coast
Timu hiyo imepangwa Kundi D lenye timu zingine za Morocco, DR Congo na Zambia katika fainali za AFCON
Advertisement

Kocha wa kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars', Adel Amrouche, amesema wanaendelea vizuri na maandalizi yao kuelekea michuano ya Afcon nchini Ivory Coast huku wakiwa na ratiba ya mazoezi mara mbili kwa siku.

Advertisement

Akizungumza akiwa nchini humo, Amrouche amesema tangu walipofika Jumatatu kikosi kimekuwa kikiendelea na ratiba walizopanga na amefurahi kuona wachezaji wote wakiwa katika hali nzuri ya kiushindani.

"Tunaendelea vizuri na ratiba zetu kama tulivyopanga, tuna ratiba ya kufanya mazoezi mara mbili kwa siku na ninafuraha kuona wachezaji wakiwa bado katika hali nzuri," amesema.

Stars wamefikia katika Mji wa San Pedro ambapo watacheza michezo yao mitatu ya hatua ya makundi dhidi ya Morocco, Zambia na DR Congo.

Advertisement

Maandalizi ya Stars yalianza tangu wakiwa Tanzania ambapo waliweka kambi fupi visiwani Zanzibar kabla ya kurejea Dar es Salaam na kwenda Misri ambapo walikaa kwa wiki moja.

Kikosi hicho kilihitimisha kambi ya Misri kwa kucheza mechi ya kirafiki dhidi ya Misri ambapo walikubali kichapo cha mabao 2-0 siku ya Jumapili.

Advertisement
Advertisement
More from Pulse Sports Uganda